0

HATUA 5 ZA KUZUNGUMZA NAMPENZI WAKO ALIEKASIRIKA
***

Kwenye mapenzi kuna nyakatiza kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawaida kipindi hiki huwa ni cha hatari kwasababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanyenini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefurikwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi napengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasayule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua zakuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafukona kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika.

MPUNGUZE MHEMKO.

Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtumwingine akija na busara zakutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa.

Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia nakumkubalia lawama zake. “Basimpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwaniatajiona mshindi.

MSOME SAIKOLOJIA YAKE.

Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukishafahamu hilo chukua jukumu lakumsoma kisaikojia ili kujuakama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira. 

Zoezi hili linaweza kuchukuasaa kadhaa na wakatimwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara yaku kasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “Jua nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira.

MRUHUSU AKUJIBU.

Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwaumedhamilia.” Usiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake. 

EPUKA MARUMBANO.

Kama nilivyosema hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena. “Kwa hiyo ulikuwa unasemaje… nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwacheaseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano.

MUOMBE MSAMAHA.

Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kuwa mazungumzo ilikuwa nikuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekirikosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. "Mpenzii inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane".

Bilashaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza nakuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako.

Post a Comment

Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo

 
Top