Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama ; yaishe,basi samahani,umeshinda,sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili).
Jinsi yakutumia samahani kiusahihi
Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana
zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa
mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima,
pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana
unajali.
Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana
wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. Kama ulikua
haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako
katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na
ulinganishe na hatua ulizozifanya.
Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku
unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za
midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha
ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest
forgiviness .Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni
rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi
yakujitetea ilihali umetenda kosa.
Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya
kudai msamaha. Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa
kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na
uwepo wake katika maisha yako. Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati
unamplease mpenzi wako.Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa
pindi tu unapomletea zawadi. Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake
atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au
umetenda kosa gani tena.
Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama
KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke
mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba
msamaha.
Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi
- Kubali kosa pale ambapo umetenda,(note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa)
- Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa
- Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe)
- Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo
- Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; ''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea.
Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano
wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. Timiza
malengo yako,jiheshimu,kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda
kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja.
Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo