Sauti siku zote ina maana kubwa sana katika mtiririko wa wewe kujua mwenzako ana maanisha nini.Sauti vilevile inaweza kukupa picha ya mzungumzaji jinsi alivyo kutegemeana na ongea yake.Sauti huwezesha lugha yako unayoiwasilisha kueleweka vizuri kwa msikilizaji endapo utaitumia ipasavyo.
Je wajua sauti ya mtu kwa harakaharaka inamtambulishaje kwa msikilizaji?
• Mpole
• Mkali
• Hekima na busara au
• Hasira
Linapokuja suala la mahusiano,ni vizuri uzingatie matumizi ya sauti kutegemeana na muda na hali Fulani ya maongezi.
Pale mnapokoseana, ni vizuri ukatumia sauti yako kumshusha mwingine ili
muweze kufikia muafaka.Ukiendeleza sauti ya ukali hatakama haumaanishi
kubishana, si rahisi kufikia muafaka sanasana mtaishilia kuchukizana
zaidi.
Sauti hutumika katika kubembeleza ,yale mahadhi yakupanda na kushuka kwa
sauti yako humjengea mtu hisia na ladha Fulani tofauti na unapokua
katika maongezi ya kawaida au ya wewe na rafiki yako.
Unapokua na mpenzio hakikisha unatumia sauti yako ipasavyo katika
kunakshi maongezi yenu na kuyafanya yawape furaha nakuwa na hamasa zaidi
ya muendelezo wa mazungumzo au shughuli nyingine bila kuchoka.
Siimaanishi uige sauti ya Fulani,hapana.Bali kuwa mbunifu wa utumiaji wa sauti yako.
Kuwa miongoni ya wale ambao wanapendwa kusikilizwa na wapenzi wao,sio
kwa ajili ya mapenzi ya dhati tu ,bali kwa jinsi wanavyoteka nafsi ya
mwenziwe kwa matumizi mazuri ya sauti yanayoipamba lugha na maongezi kwa
ujumla.
Nadhani ulishawahi sikia mtu anasifiwa kwa jinsi anavyoongea au umewahi
kumsikia wewe binafsi na akakufanya uvutiwe na ile hali.Jua
unavyopangilia sauti yako ipasavyo kutokana na mazingira na aina ya
mazungumzo unapokua na mpenzi wako; unamvutia (draw attention) na ni
rahisi kwa yeye kukusikiliza and act accordingly….Una maoni yako juu ya
sauti?…tupia hapa
Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo