Usikubali kuogopa kumuonyesha mke wako au girlfriend wako unampenda kisa
unaogopa washkaji au ndugu watakusema umekaliwa naye.
Ni tabia mbaya
sana unakuta mtu mzima eti anajitamba mbele za wanaume eti "mimi bwana
mwanamke hawezi niuliza niko wapi" sasa ndugu yangu wewe ndio
ulimtongoza mwenyewe tena ulimsumbua hasa msichana wa watu leo hii
anakupigia simu anakuuliza uko wapi unaanza kupanic. Tusifanye vitu ili
kuwaridhisha washkaji huko
viringeni...tufanye vitu kuwaridhisha wake
zetu.... imefikia wakati mwanaume usipokaa bar mpaka saa nane au saa
saba usiku unaonekana bwege na ukiangalia ligi ya ulaya sebleni kwako na
mke wako unaonekana bwege pia...au usipokua na demu wa nje eti wewe sio
mjanja. huu ni upuuzu tubadilikeni jamani. ndio sikatai usikae na
washkaji lakini usipitilize sasa. Naona huruma sana unakuta mtu kavaa
lipete likuuubwa la ndoa amekaa bar kwenye kiti anasinzia..jamani ?
Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo