0
 
Katika Mapenzi kuna vitu vingi unaweza kumfanyia Mpenzi wako ukamfurahisha na kumfanya azidishe Mapenzi ila katika safu hii nitazungumzia Mambo machache muhimu yatakayokusaidia kuboresha na kudumisha penzi lako kwa umpendae
YAFUATAYO NI MAMBO MUHIMU YANAYOZIDISHA UPENDO:
1.KUMNUNULIA ZAWADI MPENZI WAKO:
»
Zawadi ni moja ya sehemu husika katika Mapenzi inayoweza kufanya penzi likawa bora na lenye kupendeza siku zote, faham kwamba hakuna mtu asiependa kupewa zawadi na kila anaepewa zawadi siku zote hujihisi kama ni mtu anaependwa na anaejaliwa na kuthaminiwa hususani katika ulimwengu wa Mapenzi unapompa mpenzi wako zawadi basi faham ya kwamba utamfanya mpenzi wako ajione kama ni wapekee kwako na anathamani kubwa kwako hivyo hatosita kudhihirisha mapenzi yake kwako,
kikubwa zingatia pindi unaponunua zawadi kwa ajili ya kumpa mpenzi wako jitahidi kuwa mbunifu na uwe ni mwenye kubadilika sio kila siku zawadi zile zile zinajirudia kwa kufanya hivi utamboa mpenzi wako kuwa mbunifu na jaribu kumpa mpenzi wako zawadi zenye kutunzika mfano kama Card, maua, nguo n.k. Utamfanya azidi kukupenda zaidi na zaidi.
2. MSIFIE MPENZI WAKO:
»
Sifa zinaleta changamoto katika mapenzi. Unapaswa kutambua kuwa usiwe mchoyo wa sifa kwa mpenzi wako usisubiri watu wapembeni wamsifie mpenzi wako pindi anapofanya jambo zuri na lenye kupendeza chukua nafasi hii wewe kama kioo chake unadhani usipo msifia mwenza wako unataka nani amsifie?! Jitahidi kudhihirisha sifa kwa mpenzi wako kwa mfano umemuona mpenzi wako kapendeza basi usisite kumwambia "Sweetie nimependa vazi lako la leo ama hakika umetoka sex nakutamani zaidi ya siku zote navyokutamani ingawa siku zote unaziteka hisia zangu ila leo ni zaidi" unaweza kumpa maneno kama haya na mengine mazuri ya kuvutia, sifa zipo nyingi mbali na kumsifu mavazi yake hata tabia n.k. Kwa kufanya hivi utamfanya mpenzi wako azidishe mapenzi kwako kwani atahisi kampata mtu anaejali ubora na uhalisia wake kimaumbile na kimatendo. ZINGATIA:- Usitoe sifa ilimradi sifa zisizo na ukweli.
3. EPUKA KUMUUDHI MPENZI WAKO:
»
Sote tunafahamu kuwa hakuna binadamu aliekamilika na hakuna alietolewa nyongo kila mtu anakasirika na anakosea ila solution kubwa ni kudhibiti hasira na kurekebisha makosa na kusuluhisha hususani kwenye mapenzi, katika mapenzi hakuna jambo baya linalopunguza upendo kama ugomvi na kumuudhi mpenzi wako mara kwa mara. Ili kuboresha mapenzi na kulifanya penzi lako liwe imara na lenye kuvutia basi jitahidi kuepuka kumuudhi mpenzi wako na pindi ikitokea umekorofishana na mpenzi wako jaribu kutafuta suluhu mwite kaa nae muombe samahani iwapo kama unakosa na hata ikitokea kosa si lako pengine kakuudhi na bado unamuhitaji usikae na kinyongo wala usiumize nafsi yako kaeni muyamalize muendeleze mahusiano yenu na msiwe watu wa kuzungumzia tofauti zenu kwa watu wa pembeni. Kwa kufanya hivi daima mtakuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na mapenzi yenu hayatofika kikomo zaidi yataendelea kushamiri.
4. MFANYIE YATAKAYO MFURAHISHA:
»
Kuna mambo mengi mazuri na yakuvutia katika mapenzi unaweza kuyafanya kwa mpenzi wako yakamfurahisha kwa mfano unaweza kusoma tabia ya mpenzi wako na ukajua ni nini anapenda na kipi hapendi kufanyiwa ukajitahidi kujilinda kumtendea asiyoyapenda na ukaufungua moyo wako kwa kumridhisha kumfanyia kile anachokipenda. Katika mapenzi watu wengi hupenda kutolewa Out, kupewa ofa ya lanch, kupewa zawadi zenye mvuto na zenye hamasa nzuri kwenye mapenzi. Unaweza kufanya vitu vizuri vyenye kuvutia kwa mpenzi wako vikamvutia ikawa ni nafasi nzuri kwako kumfanya azidishe mapenzi.
5. KUWA MTU WA UTANI KWAKE:
»
mpenzi msomaji ninapozingumzia mapenzi na maanisha mazoea yaliyoambatana na upendo, siku zote mapenzi hujijenga moyoni kwa mtu kutokana na ukaribu na mazoea yaliyopo baina ya watu wawili, katika pointi hii ya mwisho nataka nizungumzie utani katika mapenzi unafaida gani. Mpenzi msomaji fahamu yakuwa utani ni moja ya sehemu katika mapenzi na utani unasaidia kuboresha mapenzi ila utani ninaotaka kuuzungumzia hapa ni utani wa kawaida na sio ule wa kuvuka mipaka. Elewa wazi kabisa unapokuwa na mpenzi wako na ukawa ni mtu wa utani inakusaidia wewe kumfanya mpenzi wako akuzoee na awe anajisikia kuwa karibu nawewe muda wote kwani utakuwa unamfurahisha kutokana na utani wako. ZINGATIA:- Usivuke mipaka ya utani, usimtanie kupitiliza, mtanie kutokana na mazingira, usiwe utani unaofanana nakweli, mtanie kwa faida.

MPENZI MSOMAJI WA BLOG HII UKIZINGATIA HAYA MACHACHE YALIYOANDIKWA NA UKATEKELEZA KAMA ILIVYO AGIZWA SIDHANI KAMA PENZI LAKO KWA UMPENDAE LITATETEREKA NA KUTAWALIWA NA SUMU YA PENZI. Siku zote Penzi litabaki kuwa imara na lenye kuvutia kwako na kwa watu wa pembeni. Mapenzi sio mitishamba dawa ya Mapenzi unayo wewe mwenyewe.

Post a Comment

Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo

 
Top