HABARI za leo wasomaji wangu? Kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda
kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mungu kwani ameniwezesha kufika siku
hii.Mada leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke akifanya ngono bila
kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.
Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya
utoaji mimba na kutupa watoto na hata kuwa na watoto wa mitaani
yanasababishwa zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa.
Mimba nyingine zinaingia kwa sababu mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga asipate.
Mimba nyingine zinaingia kwa sababu mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga asipate.
Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko
hiyo iko katika makundi makuu matatu ambayo: Mzunguko mfupi wa siku 25
kurudi nyuma, mzunguko wa kawaida wa siku 28 na mzunguko mrefu wa
siku30-35.
Wanawake wengi mzunguko wao huwa ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndiyo leo nitawaongelea zaidi.
Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu
kuanzia siku ya kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona
damu ya hedhi ya mwezi unaofuata. Kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe
15 Oktoba basi hiyo ndiyo siku yako ya kwanza.
Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza
kushika mimba ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi
siku ya 16 kama atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.
Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini akifanya ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa kudumu kwa masaa 24 hadi
48 baada ya kujamiiana hivyo kama mwanamke atafanya ngono tarehe 12
na yai likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo
zitarutubishwa.
GPL
Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.