1. Wapendwa wanaJF, kwa wale waliowahi kupitia
hatua ya uchumba hadi kufikia ndoa au hata wale ambao hawajawahi kupitia
hatua hizo, lakini wameona mifano kadhaa kwenye jamii, watakubaliana na
mimi kwamba ndoa nyingi "zinaumwa" na zinahitaji kutafutiwa "chanjo" au
"tiba!"
2. Naamini kwamba kabla ya kufikia ndoa wachumba
huwa wanavumiliana na kupendana mno, kila mmoja anamwona mwenzake ni
bora kuliko yeye! In fact kama hawajaonana siku inakuwa haijaenda sawa!
3. Lakini baada ya kuingia kwenye ndoa mambo hubadilika taratibu na kuanza kuleta kero, malumbano yasiyoisha, huzuni zisizoisha, ngumi, mateke, n.k. Kuna baadhi ya wachungaji huwa wanatumia usemi huu ufuatao wakati wanafungisha ndoa: "Wengi wa walio ndani (ya ndoa) wanaka watoke na walio nje (ya ndoa) wanataka kuingia!" Kwa maana hiyo ndoa ni taasisi ya ajabu sana!
4. Swali langu ni kwamba kwa nini uvumilivu, upendo, huruma, kujaliana, (ambao mimi nimeuita "utamu") nk ambako kunaonekana kwenye uchumba usiendelee hata wakati wa ndoa?
5. Lengo la mada hii ni kujaribu kuwasaidia wenzetu ambao wanataka kuingia kwenye ndoa pamoja na wale walioko kwenye ndoa ili waweze ku-"think twice" na kutengeneza mahusiano yao ili maisha yao yawe na ushuhuda mbele ya jamii na watoto (kama wamefanikiwa kuwapata).
6. Kwa kuanza kutoa maoni, kwa
upande wangu naona
kwamba (a) wengi wanaingia kwenye mahusiano kwa sababu ya "tamaa za
mwili" kiasi kwamba wanaangalia uzuri wa nje zaidi kuliko wa ndani!
Uzuri wa nje ukishaanza kuchuja upendo nao unaanza kuchuja vile vile!
(b) Kingine ni kwamba baadhi ya watu (hapa nafikiri ni wengi zaidi) huwa
wanaingia kwenye mahusiano kwa sababu ya kuangalia vipato zaidi kuliko
upendo wa dhati, uchumi ukianza kuyumba, ndoa nako inaanza kuyumba na
hatimaye kuvunjika!
USHAURI: Upendo wa kweli usiathiriwe na mazingira: uzuri, kipato na kadhalika! Hii ni sumu mbaya katika ndoa! Naomba maoni yenu zaidi.
Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo