0

 
Watu fulani wanasema, ukitaka nikwambie wewe ni wa tabia gani, nionyeshe rafiki zako ni akina nani, ila mimi nina sema, ukitaka nikwambie wewe ni mtu wa namna gani, nionyeshe mwanaume anaye kuibia demu,mke,au mchumba wako, au hata kama hauibii basi mwanaume anaye mpenda kwa dhati mwanamke ambaye na wewe unampenda kwa dhati.

Mnamo mwaka 2005, niliingia katika mahusiano na mdada ambaye alikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine, makubaliano yetu mimi na yule mdada yalikuwa, niweke ukuta kati yangu mimi na yule jamaa ili asije akanifahamu kwa namna yoyote ile. Kadri siku zilivyo kuwa zinazidi kwenda nikajikuta nagundua mimi na yule jamaa tuna vitu zaidi ya kimoja vinavyo fanana sana. Mifano..

1. Wote mimi na yeye ni mashabiki wa Yanga.

2. Uingereza, wote tunaipenda Arsenal.

3.Wote tunaupenda muziki wa Hiphop.

4. Wote tunamkubali Biggie kuliko Tupac.

5. Hapa Tz wote tunamkubali sana msanii mmoja wa Hiphop(jina kapuni ).

6. Wote tunapenda aina za muvi zinazo fanana...
7. Wote tunapenda rangi zinazo fanana,.
8. Wote tunaikubali CHADEMA.
9.Wote hatuipendi CCM.
10. Wote tunawachukia polisi etc

Mwisho wa siku nikaja, kuconclude that, mimi na yule jamaa, tutakuwa tunafanana kwa kiasi kikubwa sana, ndio maana basi hata katika suala la mahusiano, tumejikuta tukiwa tumefall in love kwa mwanamke mmoja....

MY TAKE:

1. Ukitaka kujijua wewe ni mtu wa aina gani, tazama tabia za mwanaume anaye kuibia demu, mke, mchumba wako ama hata kama hakuibii basi angalau anamtongoza/anampenda kwa dhati......

2. Kwa wasichana,, usimkatae mwanaume anaye onyesha kukupenda kwa dhati, eti kwa sababu upo katika mahusiano na mwanaume mwingine! U know why? kwa sababu wote mtakuwa mnaunganishwa na ufalme mmoja, " love kingdom". ufalme hauwezi kuuangusha ufalme wenzake...

Post a Comment

Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo

 
Top