Hivi karibuni nimeongea na mchungaji wangu ambaye amenishauri niendelea kumwomba Mungu na kufunga lakini hii hainisaidii kwasababu bado naendelea kutoka nje ya ndoa.
Najua natakiwa kuacha lakini sijui ni vipi. Tafadhali nisaidieni

Najua story yangu itawafanya watu wengi wanifokee lakini nitashukuru kwa msaada wowote nitakaoupata. Niliolewa na mume wangi April 2010. Ingawa kwa mara ya kwanza sikuwa na nampenda mume wangu, lakini nilikuwa nazidi kuzeeka na sikuweza kumpata mwanaumbe yeyote wa dini yangu na kabila langu, wazazi wangu walinitambulisha kwa huyu mwanaume na kunilazimisha niolewe nae.

Mara ya kwanza natoka nje ya ndoa ilikuwa bahati mbaya. Nilikutana na mpenzi wangu wa zamani na tukabadilishana Pins zetu za BlackBerry. Huwa tunachat mara zote na nikaanza kutoifurahia ndoa yangu kwahiyo nikamshawishi huyu ex wangu. Tukaanza kukutana na kuanza kufanya mapenzi. Baadae akahamia kutoka huku mjini na kuhamia mji wa mbali na hatimae mahusiano yetu yakaishia hapo.


Kutoka hapo nimekuwa na mahusiano na wanaume wengine wane ikiwemo mume wa rafiki yangu. Nina watoto wawili na mume wangu lakini siridhiki katika mapenzi.

Mume wangu ni mpole na ananipenda, na nimetokea kumpenda lakini nashindwa kuacha mahusiano yangu ya nje ya ndoa. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba mume wangu hajui chochote kile kinachoendelea. Simpi nafasi yoyote ile ya kuwa na wasiwasi na mimi. Nafuta sms zote kwenye simu yangu ingawa huwa hana tabia ya kuchungulia kwenye simu zangu. Nahakikisha hagundui chochote kwasababu nataka familia yetu isisambaratike.

Hivi karibuni nimeongea na mchungaji wangu ambaye amenishauri niendelea kumwomba Mungu na kufunga lakini hii hainisaidii kwasababu bado naendelea kutoka nje ya ndoa.
Najua natakiwa kuacha lakini sijui ni vipi. Tafadhali nisaidieni
 
Top