NANI
asiyependa furaha? Wengine wanapenda michezo, kucheza dansi au kuwa
pamoja na watu wawapendao. Lakini kwa baadhi yenu, kuwa na furaha ni
kuwa karibu na mpenzi wako. Hata hivyo kuwa karibu na kufurahi na mtu
unayemzimia, haimaaminishi lazima mjamiiane
Kushikana mikono, kukumbatiana, kupapasana au kubusiana na mtu unayempenda kunaweza kutosha sana. Vitendo hivi vinawaleta karibu zaidi na kila mmoja wenu anaweza kukidhi hisia za kujamiiana. Utaratibu huu ni salama na unatosheleza ili mradi wote mnakubaliana na mnajua wakati gani wa kuacha na kurudi nyuma! Vitu vingine mnavyoweza kufanya pamoja ni:
Kushikanashikana na kutekenyana
Kuzungumzia masuala ya kujamiiana
Kusikiliza muziki au kudansi pamoja
KUJICHUA PAMOJA
Kujichua au kusaidiana kupiga punyeto ni njia nyingine salama ya kupunguza hamu ya kujamiiana na wakati huo huo kujiepusha na mimba zisizopangiliwa, magonjwa ya ngono na Virusi vya Ukimwi. Unaweza kutumia mikono (na kondomu au bila kondomu) kusugua uke/uume wako kwenye mwili wa mwenzio usio na michubuko mpaka hapo utakapofikia raha yako. Kujichua ni salama iwapo mtahakikisha hakuna muingiliano wa manii au maji maji ya uke. Epuka kutumia vitu vyenye kemikali ambavyo vinaweza kuchubua ngozi zenu.
Kumbuka!
Kutofanya mapenzi kabisa ni njia pekee ya uhakika ya kujikinga na magonjwa ya ngono, Virusi vya Ukimwi na mimba zisizopangiliwa. Unaweza kutumia njia hizi BADALA ya kujamiiana na kuhatarisha afya na maisha yako.
KUJAMIIANA SALAMA
Kujamiiana kwa usalama kunamaanisha kujiepusha kuambukiza au kuambukizwa magonjwa ya kujamiiana na Virusi vya Ukimwi. Maana yake kuwa salama na ishi!
CHUMVI CHUMVI!
Kunyonya au kulamba sehemu za siri (uume au uke) wa mpenzi wako ni aina nyingine ya kufanya mapenzi salama. Baadhi ya watu wanafurahia kunyonya au kunyonywa lakini watu wengine hujisikia vibaya na hawapendi. Hivyo, ni muhimu kufikiria kama mwenzako kweli anataka kunyonya au kunyonywa. Msichana hawezi kupata mimba kwa kumnyonya mvulana, hata kama atameza manii yake.
JIEPUSHE NA HATARI
Unaweza kuambukizwa baadhi ya magonjwa ya kujamiiana wakati unaponyonya hususan kama una vidonda au michubuko mdomoni.
Hakikisha shahawa na majimaji ya uke hayaingii mdomoni mwako
Hakikisha kuwa mdomo wako ni salama na huna fizi zenye kutoka damu, vidonda ama michubuko mdomoni kutazidisha hatari ya maambukizo
Mwanaume anaweza kuvaa kondomu ili kupunguza uwezekano wa kusambaza maradhi na siku hizi kuna kondomu maalumu za kufanya mambo kuwa mazuri na salama!

Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo