MPE MUMEO ANACHOHITAJI.WANAWAKE wengi wanashindwa kujua wao wanatofautiana na wanaume kwa
hisia na hata mawazo ya mapenzi. Wanaume wana mambo wanayoyapenda kutoka
kwa wake zao hasa katika masuala ya mapenzi. Kwanza wanawake wajue
wanaume wengi wana hisia za haraka za kufanya mapenzi kuliko wanawake.
Mwanaume alivyoumbwa ni kwamba akiona tu mfano mwanamke umevaa kanga
moja au umevaa night dress hiyo inatosha kusisimua. Wapo wanawake
wanaowasisimua waume zao bila wao kujua. Mfano umevaa tu kanga moja au
night dress ndani huna kitu.
Kwako ni jambo la kawaida lakini kwa
mwanaume sio la kawaida kwa kukuona hivyo tayari unakuwa umeamsha hisia
zake. Ukimwona anakuja kutaka haki yake usidhani anakusumbua. Ujue
tayari mwenzako alishafiria mbali zamani we huna habari.
Ni
vyema ukawa mwangalifu kujua hisia za mwanaume huyo mumeo kama
inawezekana mpe anachohitaji kwani usipofanya hivyo unamwathiri
kisaikolojia na anaweza kufikiria nje. Wanawake wengi wa nje waliowaweka
waume zenu kiganjani hiyo ndio mbinu wanayotumia.
Akiwa na ahadi na
mumeo atamkuta kanga moja au amevaa night dress na kila anachohiji
atapewa haraka tena kwa madoido. Kwanini akitaka hayo hayo kwa mkewe
hapewi je ana kosa gani anapofikiria nje?
NB: Nikisema mpe
mumeo Hitaji lake sina maana Umpe mpaka kinyume na maumbile Ukiona Mumeo
kafikia hapo Huyo Hafai si Mume mwenye Busara huyo na wala hakutakii
mema mkatalie na Umwelimishe madhara ya Tendo la ndoa kinyume na
maumbile.
MVUTIE MUMEO KWA MWENEKANO WAKO.Mvuto ni
muhimu sana kwa mwanaume. Wanaume wanapenda wanawake wanaowavutia
kihisia. Niwaambie wanawake mlioolewa jueni kumvalia mumeo mavazi
yanayomvutia.
Sio vibaya kama nilivyosema hapo juu ukavaa kanga
moja kama upo pamoja nae. Kama nilivyoeleza hapo juu mwanaume anasisimka
kwa kuona. Kwanini avaliwe kanga moja na wanawake wa nje wakati wewe
unaweza kuvaa.
Wanawake jueni hili mnapokuwa karibu na waume
zenu jianchieni Kwa mfano hakuna ubaya wakati mumeo karudi kutoka kazini
akiwa amechoka, wakati unampotengea chakula ukavaa kanga moja au
night dress.
Unaweza kuona hilo ni jambo dogo lakini kisaikolojia
utakuwa umefanya jambo kubwa. Hapo hata kama atakuwa ameudhiwa kazini
atasahau na kukuona wewe mpenzi wake.
Usafi panga vitu vyako vya chumbani vizuri:
Jambo hili limekuwa lizizungumzwa sana hadi wengine wanasema mwanamke
usafi.
Kisaikolojia mpangalio wa vitu ndani na hasa chumbani kama ni
mbovu unaweza kuathiri hata tendo la ndoa. Kama chumba ni kichafu vitu
havijapangwa vizuri kisaikolojia kunapunguza msisimko wa mapenzi na hata
kumfanya mwenzako achukie kufanya na wewe tendo hilo ukadhani
hakupendi.
Mwanamke tandika kitanda chako vizuri panga chumba
chako tandika shuka nzuri. Siku hizi kuna shuka zina maneno ya mapenzi
nunua hiyo uwe unatandika. Kisaikolojia utamfanya mpenzi wako avutiwe
chumba chako na hata wewe mwenyewe.
Mazingira mazuri yatamfanya asisimke
haraka kimapenzi anapokuwa na wewe na hata kuitamana nyumba yake na
kurudi mapema nyumbani.
Jinsi chumba kilivyo rafu ndiyo
wanasakolojia wanasema kunafanya ubongo uwe rafu hata kuchukia.
Unaweza
kumwona mwenzako anachukia kumbe ni kutokana na mpangilio mbovu wa
chumba ndio sababu inayomfanya achukie.
Uwe msafi wa mwili:
Sio usafi wa chumba pekee unatosha pia na usafi wa mwili wako ni
muhimu.
Niwakumbushe wanawake hakuna kitu kinachowachukiza wanaume kama
mwanamke mchafu. Asiyejipenda. Sio lazima ujirembe sana lakini jitahidi
ukawa msafi. Oga vizuri paka mafuta au lotion yako jipulizie manukato
kidogo yanayomvutia mumeo.
Sio lazima utumie gharama kubwa usafi wa
kawaida unatosha na kupaka rotion kuna fanya ngozi ya mwanamke ikawa
laini inayovutia wanaume wanapenda sana wanawake wenye ngozi laini yenye
kuvutia inaleta msisimko mumeo anapokuwa anakuangalia mara kwa mara.
Wanawake wa nje hawana zaidi ya hayo ni hayo hapo juu na mengine ndiyo
wanayotumia kuwaweka waume zenu kiganjani. Usijaribu kwenda kwa mganga
hakuna atakachokusaidia memeo atatoka kama wewe humsisimui, hupangi vitu
vyako vizuri na pia kama unaendekeza uchafu ni rahisi mumeo kufikiria
nje.
Kujiamini kwako iwe ni kwa sababu unajua ‘kumhendo’ mumeo
kwa kumpa mapenzi ya kiwango cha juu, kumheshimu, mjali na kumpatia
mambo ya msingi ambayo anastahili kuyapata kutoka kwako. Ukifanya hivyo
utaifanya roho yake imsute kila anapotaka kukusaliti.
Hiyo
ndiyo iwe sababu ya wewe kujiamini na wala huna sababu ya kujinadi kwa
wenzako. Tambua kuwa kuna wanaofikia hatua ya kuhatarisha maisha yao kwa
kutoa ‘mtandao’ wakijua kuwa ni njia ya kuwashika waume zao kumbe
wanajitafutia matatizo makubwa.
Wapo waliopoteza fedha zao
nyingi kwa kwenda kwa waganga ili waume zao wasifurukute mbele zao
lakini imekuwa kazi bure. Shituka leo, anza kutumia mbinu sahihi za
kuishikilia ndoa yako na usijidanganye kwa kufanya mambo ambayo ni sawa
na kutwanga maji kwenye kinu.
Mwanamke aliyekamilika ni yule
anayeuthamini mwili wake, sasa kwa nini leo hii ukubali ‘kumrukisha
ukuta’ mumeo ili kumfanya asiende nje ? Kwa nini utumie fedha zako kwenye
kumtafutia limbwata mumeo wakati wewe mwenyewe ni limbwata tosha ?.
Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo