Kila binadamu hupenda jambo fulani. Mapenzi ya mtu juu
ya jambo yaweza kumvutia kiasi kwamba anaweza kupoteza welekeo wa maisha yake.
Watu hupenda hadi kileleni. Hapa ndipo mtu aelewi hili wala lile. Hali hii si
tu kwa vijana wanaoingia katika umri wa balehe bali hata kwa wale waliovuka
umri huu. Kweli kila mtu anahaki ya kupenda. Na mapenzi haya yalianza pale
binadamu walipoanza kuishi pamoja kama mke na mume kama vitabu vyetu vya dini
vinavyoelekeza, ambavyo ni Biblia na Kuruhani.
Napenda kuwa muwazi sana juu ya aina ya penzi
ninalozungumzia. Ni yale mahusiano ya kimwili yaliyopo kati mwanamke na
mwanaume. Haya ndiyo mahusiano ninayozungumzia na sizungumzii yale ya watu wa
jinsia moja. Mapenzi hayauzwi na ayachagui rangi wala kabila.Mapenzi ni kitu
asilia ambacho humkuta mtu juu ya mtu
mwingine ambaye anaweza kuwa mwanamke kwa mwanaume au kinyume chake. Na hawa
kila mmoja hutokea kumpenda mwenzake mpaka kufikia kilele cha penzi.
Angalia mfano huu; umepita wapi na kutembea mikoa
mbalimbali au wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa mingapi? Umekutana na
wangapi wazuri (wanawake au wanaume), na ulimpenda yupi. Inawezekana kati ya
uliowachagua hakuna hata mmoja kati ya wale uliokutana nao ukaridhia kuwa naye.
Lakini ulikutana na kijana mmoja ambaye amekuvutia sana zaidi ya asana na
mahusiano ukaanza kuanzisha mpaka leo ni mke wako au mchumba wako. Hapo ndipo
ninaposema “love is something natural” na si kitu cha kubahatisha tu.
Na ieleweke
kwamba mke mzuri ni wako tu, na mme mzuri ni wako tu. Hakuna
ubishi kwa hili. Na pale unapoona kuwa mke au mme wako si mzuri basi ulikosea
wakati wa uchaguzi wako. Hapo huna budi
kuonyesha unampenda kama kitabu hiki kinavyoeleza uk.6 & 7. Na ujue kwamba
kila mtu ana haki ya kupendwa na mme, mke au mchumba wake. Penye upendo pana mapenzi ya kweli.
Kazi hii imeandaliwa na
CHIWAMBO, A. R. (2011)
BA SOCIOLOGY
TEOFILO KISANJI UNIVERSITY (TEKU).
Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo