Katika
ulimwengu wa mapenzi hakuna Jambo linaumiza Roho na Moyo kama kuachana na
Mpenzi wako ambae ulimpenda kwa dhati na kuhisi ndie aliestaili kuwa chaguo lako katika maisha
ya hapa Duniani.
Suala
la kuachana limeumiza watu wengi wanaume kwa wanawake vijana kwa
watu wazima na hili hutokea tu kwa wale watu ambao hawakujiandaa kuachana au
kupokea taarifa ya kuachana au kutengana,kwa mujibu wa tafiti mbali mbali
zilizofanywa zinaonesha sailimia kubwa ya wanawake huumia zaidi pindi
wanapoachwa kuliko wanaume,nah ii inatokana na ukweli kwamba wanaume wanakuwa
wameshaa tayarisha mazingira baada ya kuachana.
Kila mmoja anatambua kuachana
si jambo jema katika maisha ya mahusiano
lakini kuna wakati hunabudi kufanya maamuzi haya mazito kutokana na ukweli
kwamba unakuwa umechoshwa na tabia,mwenendo au hata maisha ya huyo mpenzi wako
labda amekuwa mwongo sana,msaliti mnoo,msherati na tabia nyingine nyingi zisizo
stairi na kuweza kukuletea matatizo katika maisha ya kila siku ya hapa Duniani.
Leo Mpita
Njia nakuletea njia chache kati ya nyingi ya kuweza kuachana na mpenzi wako
pasipo kuumia Roho kama ifuatavyo.
1.JIULIZE KWANINI
UNATAKA KUACHANA NAE
Ukijiuliza
kwanini unataka kufanya maamuzi hayo mazito utagundua ukweli uliojificha ndani
yake kama kweli upo sahihi kwa maamuzi hayo au unasukumwa na Hasira kufanya
maamuzi hayo,ukigundua si hasira jiulize kwanini imekuwa sasa na haikuwa siku
za nyuma ya mahusiano yenu?hapa ndipo utapopata utofauti ambao utakupa
kujiamini kwa maamuzi utayofanya,na kama utaona unakila sababu ya kuachana nae
kutokana na utofauti wenu amini kabsaa hauta umia moyo kwa maamuzi yako.
2.ANDIKA SABABU ZA
WEWE KUACHANA NAE
Ndioooo
unapaswa kuandika sababu za wewe kuamua kufanya maamuzi hayo ya kuachana nae
kwani usipotambua sababu itakurahisi kwako kuhisi maamuzi yako si sahihi lakini
ukiandika utaona haja na kusimamia katika uamuzi wako,
mfano
pengine amekusaliti mara tatu,amekudanganya sanaa,ametembea na rafiki
yako,unatumia muda mwingi kumfikili yeye,unatumia ghalama kubwa sana kuwa
nae,hadhamini upendo wako,hana mapenzi ya dhati kwako,amekutangazia mbovu kwa
rafiki zako,umekuta sms za wa watoto wa kike ktk simu yake ,unaogopa kupewa
magonjwa,hupendi kushare mapenzi nk.
ukiandika
list ya vitu hivi hakika hutaona sababu yaw ewe kuendelea kuwa na huyo mtu kwani
utajionea huruma kwa mambo mengi kiafya,kiuchumi na hata kisaikolojia.hivyo
ukifanya maamuzi hutaludi nyuma wala kuumia moyo.
3.WAAMBIE RAFIKI ZAKO
WA KARIBU
Siku
zote Rafiki wana nafasi kubwa sana ya kukusaidia kuepukana na mambo ya hatari
ila kama hao rafiki ni wazuri ,ikitokea unataka kufanya maamuzi ya kuachana na
mpenzi wako unaweza kuwashirikisha wale rafiki ambao ni msaada kwako.
maana
wao watatambua kuwa umeachana na boy wako hawawezi kukuuliza afya ya mtu
wako,au kukukumbusha mambo ambayo wanajua yatakuumiza roho na kukukosesha amani
kama utayakumbuka hivyo utakuwa umewafunga wasiweze kukukumbusha, lakini pia
rafiki hao ndio watakao kuweka busy kwa kukupigisha stori,
kuchat
na kumsahau Yule aliekupa shida kwa muda mrefu,hivyo kabla yaw ewe kumwambia
mpenzi wako kuwa wewe nay eye bhasi hakikisha unawatu au kuna vitu vya
kukufanya uwe busy hivyo nafasi yake katika akili yako itakuwa ndogo sanaa.
4.MWAMBIE AJUE
MMEACHANA
Jambo
lamsingi sana katika kufanya maamuzi ya msingi pia ni kuwa wazi kwa kila jambo
hivyo baada ya kuandaa mazingira teyari usiishie kukaa kmyaa bali unapaswa
kumwambia ukweli kuwa mimi na wewe kuanzia sasa BHASSSSSS TENA,
kwakufanya
hivi utakuwa umejiweka mahali pazuri kwani hata kutafuta kwa kujuwa yupo huru
kuendelea na mambo yake,angalizo hapa wengi wakishaambiwa hivi huwa wanakuwa
wagumu kuelewa lakini wewe simamia hoja zako kusema Enough,ikipita wakati
atapokea hali ile na kuendelea na maisha yake na wewe kuendelea na maisha yako
ya kila siku pasipo kupata bhughuza kutoka kwake na kufanikiwa lengo lako.
5.JIPANGIE SIKU NA TAREHE YA WEWE KUFANYA MAAMUZI HAYO.
Jambo
la mwisho lazima ujipangie siku na tarehe ya wewe kufanya maamuzi hayo hii itakufanya upate
nafasi ya kuweza kumtoa huyo mtu katika akili yako,mawazo yako na hata moyo
wako taratibu taratibu mpaka siku unafanya maamuzi ya mwisho moyo wako
hautashtuka kwa kuwa umeshajiandaa na hilo jambo na hautaweza kujutia maamuzi
yako hata siku moja kwa kuwa ulikuwa na kila sababu ya kuachana nae .
Nimalizie
kwa kusema kwamba katika kufanya maamuzi ya kuacha na mtu lazima uangalie vitu
vingi vinavyowazunguka na kukusukuma kufanya hivyo ili wewe uwe kati,ka hali
nzuri japo si vizuri kufanya maamuzi hayo wakati ukitawaliwa na hasira kwani hapo
utakuwa unaongozwa na hasila na si uhalisia.
Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo