Pengine hii inawahusu walio katika ndoa na ambao bado!Ni zipi hasa lugha za mwili katika mapenzi?! Hapa nnazungumizia ishara, milio au sauti fulani ambazo ukisikia au kuona kutoka kwa mwenza wako inakupasa uchukua hatua stahili kulingana na mzingira husika. Kwa wale ambao tupo katika ndoa naimani unanafasi nzuri ya kumsoma mwenza wako na kuweza kugundua anahitaji au anamaanisha nini akiwa hivyo.


Kuna baadhi ya wanawake huwa hawawezi kuwaambia waume zao kwamba wanawahitaji kimapenzi, badala yake huweza kujitegesha au kujirahisi mbele zao, kwani wanajua kuwafanyia hivyo kutaamsha hamu kwa waume zao na hatimaye kuipata starehe hiyo pamoja. Mume yakupasa uwe unausoma mchezo mapema kwani si wanawake wote wataweza sema au kujitegesha na ndio maana tunasisitiza isipite wiki bila kupeana na mwenza wako.

Pia wanawake nawashauri wawe "wachokozi" kidogo maana kuna wanaume huwa hawaanzi mashambulizi mpaka washambuliwe, kama hali ipo hivyo basi mwanamke inabidi ndo ume mpangaji mashambulizi ya awali.

Mwisho niwaambie Mke na Mume, kama inavyowapasa kujua sehemu za mihemuko baina yenu, inawapasa pia muelewe lugha za miili yenu. Miili inaongea bwanaa!!!
 
Top