Mwanamke ndivo hivi anavopenda siku zote maishani mwake
Usipende siku zote mwanamke atoe machozi yake juu yako mala kwa mala

....................................................................................................... 

  Mwanamke Akikupenda Usimdharau Kama Yeye Ni Malaya… Na Mwanamke Mpaka Ukiona Hajatulia Basi Jua Tatizo Lako Wewe, Fanya Juu Chini Ili Kuweza Kumbadilisha Kwa Sababu Kumbadilisha Mwanamke Ni Kitu Kidogo Sana Kwa Sababu Umekaa Naye Muda Mrefu Na Ni Lazima Utajua Tu Umguse Wapi Aweze Kuwa Kama Mwanzo,


Na Usijeomba Mwanamke Akulilie Machozi Mbele Zako, Ameshindwa Kumlilia Baba/Mama Yake Aliyemzaa Na Amekuja Kukulia Wewe… Wewe Una Nini? Epukana Na Hili Na Utunze Heshima Yake Na Umpe Penzi Lako, Hakuna Mwanamke Mbaya/Malaya/Kicheche Ila Wewe Ndio Utafanya Awe Hivyo… Wengi Wao Wameshawahi Kufanya Haya Na Sasa Wanalia Na Kusaga Meno Kwa Sababu Walijisahau Na Mwishowe Sasa Hawajielewi Kutokana Na Maisha Wayoishi Ya Kutokua Na Chaguzi Zilizo Za Halali…

Mwanamke Anapenda Kupendwa! Mara Nyingi Wanawake Ndiyo Hasa Huwa Na Mapenzi Ya Dhati Zaidi Kuliko Wanaume. Mwanamke Anapoamua Kuwa Na Mpenzi Wake, Humpenda Kwa Moyo Wake Wote, Hivyo Hupenda Kuwa Salama Katika Penzi La Dhati Kwako.

Anapenda Uhuru, Anapenda Kujisikia Wazi Kwako Mahali Popote. Mwanamke Anajisikia Vibaya Sana Anapokuwa Hana Uhuru Hata Wa Kukushika Mkono Mnakuwa Barabarani Pamoja. Anapenda Penzi La Uwazi!

Maana Mwingine Utakuta Akikutana Na Rafiki Yake, Badala Ya Kumtambulisha Vizuri Kama Mpenzi Wake, Anaanza Kupatwa Na Kigugumizi. Utamsikia Akisema: “Ah! Huyu Ni Rafiki Yangu Bwana, Anaitwa Latipha....”Hili Ni Kosa Kubwa Linalofanywa Na Wanaume Wengi Bila Kujua Ni Kosa.

Mwanamke Anakosa Amani Ya Moyo Kutokana Na Unavyomtafsirisha Mbele Ya Rafiki Zako. Anahisi Hayupo Salama. Lazima Atajiuliza Maswali, Kwanini Hataki Kunitambulisha? Kwanini Anashindwa Kusema Mimi Ni Mpenzi Wake? Sifananii? Sina Mvuto Au Nina Tatizo Gani?

Hayo Yanaweza Kuwa Maswali Yatakayomuumiza Sana Kichwa Mpenzi Wako, Ambaye Si Ajabu Akafanya Maamuzi Ambayo Hutayapenda. Kidonda Hiki Hubaki Moyoni Mwa Mwanamke, Huwa Vigumu Sana Kuonyesha Wazi Kwamba Amechukia Kutokana Na Uliyomfanyia, Lakini Atabaki Akiugulia Moyoni Mwake Kwa Uchungu.
Hata Hivyo, Kinachokuja Akilini Mwake Ni Kutafuta Mwanaume Mwingine Ambaye Atakuwa Wazi Kwake Ili Aweze Kufurahia Mapenzi Badala Ya Kuendelea Kuumia Moyoni Mwake. Ni Dhahiri Kwamba Uamuzi Huu Hautaufurahia Hakika.
 
Top