0
Kwa walio addicted to facebook atiii mwaambiwa to WATCH OUT! Utafiti umeonyesha kwamba ndoa nyingi zimekuwa zikifunjika kutokana na facebook na wasichana/wanawake wengi wamekuwa wakijikuta katika matatizo makubwa na kuuwawa kutokana na Facebook. Je haya yasemwayo ni kweli? Well, embu tuangalie vizuri data kwamaana lisemwalo lipo na kama halipo basi lajaaa hapo nyuma.

Ndoa - sikuhizi unaambiwa kiwango cha wanaume wenye account ya Facebook imeongezeka kwa kipimo kikubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma kidogo. Wanaume wengi wanaonekana kucheck facebook sikuhizi. Na wanawake pia hivyo hivyo, yaani kiwango cha wanao peruzi facebook kimeongezeka mmno haswa miaka ya hapa karibuni. Halafu, since facebook ni mahali pa kukonnect na watu, ndugu, marafiki na jamaa waliopotezana toka zamani. Well, katika kukutanisha waliopotezana, watumiaji wengine wa Facebook wamekuwa wakienda mbali zaidi na kutafuta wachumba wa zamani na hata wengine kuvuruga nyumba za watu.

Kuna habari moja nilikuwa nasoma ya wadada wakielezea jinsi ndoa zao zilivunjika kisa Facebook. Mmoja alisema eti, kwasababu ya kutokuwa na mapenzi mazuri nyumbani na umoja kati ya yeye na mumewe (mumewe na watoto) basi alitafuta kitu cha kumweka busy na alijikuta akitumia muda wake mwingi kwenye facebook na ndo hapo alipokutana na mchumba wa zamani ambaye baada ya mawasiliano ya muda mrefu kwa kuficha ficha, alijikuta akifall inlove naye.
 Hivyo jinsi mambo yalivyokuwa yakienda murwa basi kwa pamoja wakaamua waanze maisha yao mapya pamoja. Huyo dada aliendelea kwa kusema kwamba, mambo kati yake na jamaa wake mpya so far yanakweda safi na anafuraha aliyokuwa akiitafuta. Well, this is a rare case, na kumbuka hata kama wanamatatizo hawatasema kwasababu mh, watu watamjudge kwamba alikuwa akifikiria nini kutafuta mchumba kwenye facebook. Anyways, all in all kesi yake imeeishia pazuri. Amshukuru Mungu kwamaana kuna kesi zinazoishia vibaya mnoo.

Well, kwa upande wangu, namwish the Very Best kwamaana, hopefully asije akarudia tena huko alipotoka.
Kwamaana mara nyingi history hujirudia.
Well, tatizo ni kwamba siku hizi hakuna wa kumwamwini wedha unakutana na mtu online, kwenye facebook ama hata kwenye party au ofisini. Dunia imebadilika na Uovu umezidi. Wakati mwingine unaweza kukuta hata huyo mwanaume anayekwambia anakupenda sana, na yeye huko alipo labda hata anafamilia yake lakini ndo hivyo kutokuridhika na kutaka pembeni kidogo. Either way kabla ya kufanya mahusiano ya kupitia Online chats na Facebook, ni vizuri mtu kuwa very informed kuhusu mtu unayefanya nae/ama mtu unayetaka kuanza nae mahusiano.

Nilikuwa naongea na rafiki yangu ambaye alitokea kukutana na mtu mzuri tuu online ijapokuwa mambo yao hayakwenda vizuri at the end ila yeye pamoja na jamaa wote wamebakia kuwa na urafiki mzuri tuu wakuheshimiana however, rafiki yangu huyo alitokea kunielezea mkasa uliyomkumba mtoto wa besti yake. Mkasa ambao ulisikitisha sana na ulioacha pengo kwenye familia ya msichana huyo na ulianzia kwenye facebook. 

However, ninavyoona mie, mara nyingi hizi case za aina hii hutokea kwasababu mtu unakutana na mwanaume na all of the sudden kumwamini mwanaume katika kila analolisema. Unakuta mtu mwingine anasafiri mji hadi mji kwenda kumtembelea mtu asiye hata mjua ila tu wamekutana kwenye mtandao na wamekuwa wakiongea vizuri. Kama nilivyosema however, sio kesi zote ni mbaya ama sio kila mtu ni mbaya lakini ni muhimu kujiuliza maswali mengi kabla hujaweka maisha yako on the line kwa kumfuata mtu usiyemjua. Ni vizuri kumchunguza mtu kwanza.

Pia Facebook saa nyingine inaweza kumfanya mtu ajisikie kama vile anapitwa na kunavitu anamiss. Kutokana na picha watu wanazopost na vitu mtu anavyokuwa kijadili kuhusu maisha yake (kuparty n.k). Facebook inaweza kupotosha kama mtu hujakaa vizuri ama hujiamini. All I wanna say is that, kama unajiona uko addicted to facebook ama kunavitu vinavyokukwaza kutokana na kuangalia sana Facebook basi punguza spidi na hata kama ni lazima ifunge na pumzika kwa muda. Kwamaaa ukifuatiliana sana mambo yanayoendelea kwenye Facebook na vitu watu wanavyopost unaweza kupotea bure. 

Personally, nilikuwa addicted to Facebook kipindi wakati niko shule. Yaani ilinibidi nifunge Facebook yangu kwa muda kwamaana niliona hapa kufeli na kutopay attention kuna nukia lol. Anyway, I was just lucky to be able to detect my own addiction na nikafanya uamuzi ambao I needed to do. However, baada ya shule kuisha I was back on Facebook again ila siku hizi its a once in a while thing, naona stim ilikwisha ghafla. 

Hivyo, nilichotaka kusema tuu ni kwamba, nimuhimu kuwa makini na Facebook wedha una Facebook for fun (kuangalia watu wanafanya nini or unafacebook kutafuta wachumbaz na other networking connections). Kuna fisi wamekaa wanasubiri kudaka wale wasio makini na huwezi jua jinsi gani unaweza kuhatarisha maisha yako or all that you have worked hard to have. Bestes!

Post a Comment

Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo

 
Top