Home
»
» Unlabelled
» WADAU HII NI HATARI KATIKA MAPENZI
Aina mpya ya vimelea vya ugonjwa wa kisonono au "gono" ambavyo vinahimili dawa(resistant to drugs)
zinazotumika kutibu ugojwa huu imegundulika duniani. Taarifa
iliyotolewa na shirika la afya duniani (WHO) hivi karibuni imesema,
ugonjwa wa kisonono unaoathiri mamilioni ya
watu ulimwenguni umeanza kuwa sugu dhidhi ya dawa zinazotumiwa kuutibu na hivyo kuna hatari ya kutoweza kutibika kabisa.
Shirika la afya duniani limetoa wito kwa serikali na madaktari kuongeza
ufuatlijiaji wa aina hii ya kisonono kutokana na ugonjwa wa kisonono
kuwa
na athari nyingi kama mcharuko (inflammation), ugumba, matatizo wakati wa ujauzito na hata vifo vya kina mama wajawazito.
“Aina hii mpya ya vimelea vya kisonono vinaonyesha usugu dhidhi ya dawa
zote za antibiotiki tunazotumia dhidhi yake ikiwemo dawa za jamii ya
cephalosporins ambazo ni dawa za mwisho katika kutibu ugonjwa wa
kisonono, “ alisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan, mmoja wa wanasayansi
wa shirika la afya duniani katika kitengo cha magonjwa ya zinaa.
Miaka michache ijayo, aina hii mpya ya kisonono itakuwa sugu dhidhi ya
dawa zote ambazo tunazo saizi “aliendelea kusema Dk. Manjula Lusti-
Narasimhan wakati wa mahojiano na shirika la habari la The Associated
Press kabla WHO haijatangaza rasmi hatua na mwongozo mpya wa kukabiliana
na tishio la aina hii mpya ya kisonono.
Inakisiwa watu milioni 106 ulimwenguni kote huathiriwa na ugonjwa wa
kisonono kila mwaka.Ugonjwa wa kisonono pia huongeza hatari ya kupata
maambukizi ya ugonjwa wa Virusi vya Ukimwi (VVU).
“Ugonjwa sugu wa kisonono sio tatizo la bara la Ulaya au Afrika pekee
bali ni tatizo la dunia nzima kwa sasa,’” alinukuliwa akisema Dk.
Manjula Lusti-Narasimhan.
Kwa mara ya kwanza, vimelea sugu vya ugonjwa wa kisonono dhidhi ya dawa
aina ya cephalosporins viliripotiwa katika nchi ya Japan, ikifuatiwa na
Uingereza, Hongkong na Norway.
Wanasayansi wanaamini matumizi mabaya ya dawa aina ya antibiotiki pamoja
na uwezo wa vimelea vya ugonjwa wa kisonono kubadilika na kuzoea
mazingira mapya ndio chanzo kikuu cha kutokea kwa ugonjwa sugu wa
kisonono na hivyo muda si mrefu ugonjwa huu utakuwa janga kubwa dunia
nzima kama hatua za haraka hazitachukuliwa. Kuna uwezekano wa vimelea
hivi sugu vya kisonono vinasambaa kwa sasa duniani bila kuweza
kugundulika kutokana na nchi nyingi kutokuwa na ufuatiliaji na utunzaji kumbukumbu mzuri wa wagonjwa wake.
Shirika la afya duniani limesema nchi zinatakiwa kuongeza ufuatiliaji wa
wagonjwa wake pamoja na kudhibiti matumizi holela ya dawa za
antibiotiki mpaka pale taarifa kamili za ugonjwa huu zitakapojulikana.
“Elimu ya masuala ya kujamiana pamoja na matumizi sahihi ya mipira ya
kondomu inahitajika ili kutokomeza kabisa ugonjwa huu sugu wa kisonono.
Hatuwezi kuutokomeza kabisa ugonjwa huu bali tunaweza kuzuia usambaaji wake,”alisema Dk. Manjula Lusti-Narasimhan.
Kwa taarifa zaidi za ugonjwa huu
Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo