0

            http://cdn.madamenoire.com/wp-content/uploads/2012/04/black-couple-in-bed-spark1ne-com1-378x338.jpg

KEVIN amefanikiwa kukimbia mkono wa Jackson Motown baada ya kunusurika kuuawa huku akiwaacha Jackson Motown na washirika wake wakiwa katika hali mbaya baada ya kuwamwagia tindikali.

Amekimbia na kufikia kwa mzee Thomas Edmund ambaye baada ya kumuelewesha ni kwa nini alikuwa hapo, mzee huyo anampokea na kuahidi kumtunza. Kevin anafurahi lakini bado ana hofu, haamini kama yupo sehemu sahihi lakini mzee huyo anamhakikishia kwa kumweleza kwamba hakuna mtu hata mmoja ambaye angefahamu uwepo wake ndani ya nyumba hiyo.

Maisha yanaendelea, Kevin akiwa hapo na siku moja mzee Thomas anamuaga kwamba angesafiri kwa usiku moja kwenda mjini Miami, hofu inamwingia Kevin lakini mzee huyo anamtuliza na kumwambia atakuwa salama.
 
Upande wa pili, Jackson Motown amekamatwa na kufikishwa polisi akiwa katika hali mbaya, anaeleza kila kitu na mwisho kusema kwamba Kevin hakufa alikuwa amekimbia sehemu fulani baada ya kuwamwagia tindikali. FBI wanaondoka tena kueleka Opa Locka kwa ajili ya msako wa Kevin kwa kutumia mbwa wanafanikiwa kuifikia nyumba ambayo ndani yake ndimo alimokuwa Kevin, lakini ghafla wakiwa mita chache tu, wanashuhudia mlipuko mkubwa ulioambatana na moto, nyumba yote inateketea.
Je, nini kimetokea hapo?
 
SONGA NAYO…
PAMOJA na moto mkubwa, pia palikuwa na vumbi pamoja na moshi mzito, maofisa wa FBI na askari wakabaki wamelala chini kwa dakika arobaini na tano bila kunyanyuka, hali ilipotulia na kusikia sauti za watu wakiongea ndipo waliinuka na kuanza kujikung’uta vumbi huku wakijaribu kuangalia kupitia katikati ya moshi mzito.

Moto ulishapungua ingawa bado ulikuwa ukiendelea kuwaka, kiongozi wao Derrick Fisherman alifikia uamuzi wa kupiga simu makao makuu kuomba msaada wa wapelelezi kutoka kitengo cha upelelezi wa eneo lilipotokea tukio au kwa Kingereza Crime Scene Investigation, ili wafike na kuchunguza vizuri eneo hilo kugundua ni kitu gani hasa kilitokea na nani alitega bomu.

Haukupita muda mrefu baada ya mazungumzo hayo ya simu, gari la zimamoto kutoka Idara ya Zimamoto ya Opa Locka lilifika na kuanza kuuzima moto huo hadi ukaisha kabisa, hakuna aliyeruhusiwa kuingia ndani ya jengo hilo, lilizungushiwa uzio maalum ili kuzuia ushahidi kuharibika, yalifanyika yote hayo wakisubiriwa maofisa kutoka New York kwa ajili ya uchunguzi wa eneo husika ambao walifika saa tatu baadaye kwa helikopta.

Maofisa hao wanne waliingia ndani ya jengo na kuanza kuchunguza wakipiga picha kila kitu walichokitilia shaka na walipomaliza kazi yao, waliomba kuongea na majirani ambao walitoa maelezo kwamba ndani ya nyumba hiyo aliishi mzee Thomas Edmund peke yake.
“Tumekuta mabaki ya mwili wa mtu mmoja!”
“Atakuwa ni yeye.”
“Hakuna mtu mwingine aliyeishi humu?”
“Ni yeye tu na mbwa wake.”
“Ni kweli tumekuta pia mabaki ya mbwa.”
“Mungu wangu! Mzee Thomas amekufa masikini, nani atashughulikia maua yake?” alisema mwanamke mmoja jirani wa mzee huyo.

Uchunguzi wa maofisa hao wa FBI kwenye eneo la tukio ulipokamilika jioni ya siku hiyo, ilithibitika kabisa kuwa bomu lilitegwa na watu waliofika nyumbani kwa mzee Thomas usiku, baada ya tukio hilo waliondoka na kupotelea porini bila kugundulika, kila mtu alisikitika.

Kabla askari hawajaondoka eneo la tukio, gari aina ya Land Rover 110 ilifika ikiendeshwa kwa kasi kama vile mashindano, ikajivuta chini baada ya breki kukanyagwa na kutimua vumbi jingi, watu wengi walifahamu ni maofisa wa polisi wamefika, lakini walibaki mdomo wazi pale aliposhuka ndani ya gari hilo mzee mwenye ndevu zenye mvi nyingi akilia kwa sauti ya juu.

“Mh! Mzee Thomas? Yupo hai?” majirani walisikika wakiongea kwa sauti ya juu.
“Maskini nyumba yangu! Maskini mbwa wangu! Maskini Kevin, wamemuua!” alilia mzee huyo na kuanguka chini akiwa haamini alichokishuhudia.
“Tulifikiri wewe ulikuwa ndani ya nyumba?”
“Hapana, nilisafiri nikamwacha mgeni wangu!”
“Nani?”
“Kijana anayeitwa Kevin!”
“Mungu wangu! Basi yeye ndiye amefia ndani ya moto, unafikiri nani anaweza kuwa amefanya hivi?” Maofisa wa FBI walimuuliza.
“Hakuna mwingine isipokuwa Jackson Motown, Kevin amenisimulia kila kitu juu ya unyama ambao tajiri huyo amemfanyia na anafanya kila kinachowezekana kuhakikisha anapoteza ushahidi ili aepuke mkono wa sheria, haiwezekani, kama ni kufa basi bora tufe lakini sheria ichukue mkondo wake!” Mzee Thomas aliongea maneno hayo ingawa katika Lugha ya Kingereza.

***
“They need skin grafting and later on plastic surgery to repair their faces!” (Wanahitaji kubandikwa ngozi mpya na baadaye wafanyiwe upasuaji wa kurekebisha sura!)
“What about sight?” (Vipi kuhusu kuona?)
“Nothing can be done to make them able to see again!” (Hakuna kinachoweza kufanyika kuwafanya waweze kuona tena!)
“Oh my God! They are going to be blind forever?” (Oh Mungu wangu! Kwa hiyo watakuwa vipofu siku zote?)
“Sure!” (Hakika!)

Yalikuwa ni maongezi ya madaktari wodini kando ya vitanda walivyolazwa Jackson Motown na wenzake, hali zao zilikuwa mbaya, nyuso zao zikiwa zimetafunwa na tindikali! Haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kuwatambua! Kuharibika kwa sura hakukumuumiza sana Jackson Motown, kilichomsumbua ni kesi iliyokuwa mbele yao ya kubaka na mauaji, hakutaka kabisa kusikia juu ya mambo hayo, ndiyo maana alikuwa tayari kufanya lolote kuficha ushahidi.
Pamoja na maumivu yote aliyokuwa nayo akiwa kitandani, tena chini ya ulinzi mkali, bado aliweza kuwasiliana na watu wake wa kazi akiwatumia askari waliokuwa wakimlinda ambao tayari walishahongwa fedha ili wasimbane, walimtafutia namba ya simu ya mtu aliyemhitaji kwenye simu yake na baadaye kumsaidia kuipiga ndipo alipoweza kuendelea kutoa maelekezo kwa kundi lake la kuficha ushahidi.

“If you use dogs, you can be able to locate where that bastard is hiding!” (Mkitumia mbwa mtaweza kujua ni wapi huyo mwanaharamu amejificha!)
“We will find out!” (Tutajua alipo!)

“He is dangerous to me and my wealth, once you find out, there is nothing you can do apart from killing him!” (Ni mtu wa hatari kwangu na utajiri wangu, mkishajua alipo, hakuna mnachoweza kufanya isipokuwa kumuua!) Jackson Motown alitoa maelekezo akiwa wodini, hakuna alichotaka kusikia isipokuwa kifo cha Kevin.

Alishaua watu wengi katika kuhakikisha haingii matatani, hivyo kwake halikuwa jambo gumu au la hatari kwake kuua mtu mwingine tena. Jioni ya siku hiyo alipewa taarifa kuwa kwa kutumia mbwa walifanikiwa kugundua mahali alipojificha Kevin, ndani ya nyumba moja mita mia moja na hamsini kutoka shambani kwake.

“Whose house?” (Kwa nani?) aliuliza.
“An old man named Thomas Edmund!” (Mzee mmoja anaitwa Thomas Edmund)
“Bomb his house, he too deserves to die with Kevin!” (Lipueni nyumba yake, yeye pia anastahili kufa pamoja na Kevin!)
“It will be done!” (Itafanyika!)

Usiku wa siku hiyo vijana wa kazi wa Jackson Motown walifika tena nyumbani kwa Thomas, wakifahamu yeye pia alikuwa ndani ya nyumba hiyo na kutega mabomu yao yalipuke ndani ya saa moja wao wakiwa wamekwishaondoka, walichokisikia baadaye ni mlipuko mkubwa, mmoja wao akampigia simu Jackson Motown kumpa taarifa.
“Job done!” (Kazi imefanyika!)
“Very good!” (Safi kabisa)
Je, nini kitaendelea? Kevin amekufa? Catarina akizipata taarifa hizi atafanya nini? Fuatilia kesho katika Gazeti la Championi Jumamosi.

Post a Comment

Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo

 
Top