Habari Admin,
Naombeni msaada wa
maawazo yenu, nimegundua kuna mwanamke anatembea na mume wangu, mume wangu
alikataaaaaa kwa mara ya kwanza, lakini baada ya kufatilllia na kuchunguza kwa
muda mrefu nikaja kuhakikisha ni kweli kabisa, mwanamke anaomba msamaha kwamba wataachana
na hatorudia tenaa, na mume wangu pia anasema hatorudiaa,
Nimeumia sana
mwenzenu, nimeumia kupita kias, kwakuwa nilimpenda, nilimheshimu, nilimjali
sana mume wangu, nilikuwa teyari kumuachia yeye kila kilicho changu,
nilimsikiliza sana, sikutegemea kama atakuja kunitenda hivi, imekia kipindi
najuta kwanini niliolewa nay eye,
sikutegemea kabisa kutokana na muonekano alio nao,,, details zoote za
huyo mwanamke wake niko nazo, niliomba niprintiwe kupitia mitandao ya simu
wanayotumia, niko nazo mkononi, staki kuamini, ninalia kama mtoto mdogo, ni
bora niibiwe pesa nitatafuta, kuliko kuibiwa penzi,, nitalipata wapi,,
Nimechanganyikiwa,
nataka kuondoka kwenda kwetu nikapumzike, nimwache kwanza, maana kila nikimuona
Napata hasira natamani kumkaba kabisa, nimemchukia mno,,, sina amani ya kuwa nay
eye, hali hii hadi lini?? Nifanyaje?
Post a Comment
Kama umependezwa na hii stori toa maoni yako kama unayo