Leo nataka tujadili na kuulizana kuhusu suala hili, maana nimekuwa
niiskia watu wengi wanaliongelea kwa mitazamo tofauti, kwenu nyie
mliokuwa katika ndoa na mahusiano ya muda mrefu, mnaonaje dhana hii ya
mapenzi ya dhati na mazoea.
MTAZAMO WANGU.
Binafsi, napenda niseme haya:- Miongoni mwa mapenzi ya dhati na matamu
hujengwa na mazoea baina ya wapendanao, Mke na Mume wanapozoeana na
Kufahamiana, kunakuwa na Uhuru baina ya Wapendanao hawa, Uhuru huu
ukitumiwa vizuri kwa kuzingatia Heshima na Mipaka, wanandoa hawa
wanakuwa kama ndugu, kitu kimoja au mwili mmoja.
Na
ndio maana ikitokea wanandoa wamepata bahati ya kuona bila kufahamiana
au kujuana mwanzoni kunakuwa na maisha ya ukimya na uoga hasa kwa
mwanamke, lakini kadri anavyozidi kuishi na mumewe, humzoea na kumpenda
zaidi.
Pia kimaumbile, mapenzi ya mwanamke huja na kuongezeka baada ya kumzoea na kuishi muda mrefu na Mumewe au Mpenziwe.
Kwa kupitia hoja hizo, natetea wale wenzangu na mimi tunaosema kwamba
mapenzi ya dhati yanajengeka na mazoea, lakini mazoea hayo yawe
yanazingatia heshima na uhuru wenye mipaka.
Je wewe Mpenzi Msomaji, unaonaje...??? Nakaribisha Maoni......