Pengine hii inawahusu walio katika ndoa na ambao bado!Ni zipi hasa lugha za mwili katika mapenzi?! Hapa nnazungumizia ishara, milio au sauti fulani
ambazo ukisikia au kuona kutoka kwa mwenza wako inakupasa uchukua hatua
stahili kulingana na mzingira husika. Kwa wale ambao tupo katika ndoa
naimani unanafasi nzuri ya kumsoma mwenza wako na kuweza kugundua
anahitaji au anamaanisha nini akiwa hivyo.
Kuna
baadhi ya wanawake huwa hawawezi kuwaambia waume zao kwamba
wanawahitaji kimapenzi, badala yake huweza kujitegesha au kujirahisi
mbele zao, kwani wanajua kuwafanyia hivyo kutaamsha hamu kwa waume zao
na hatimaye kuipata starehe hiyo pamoja. Mume yakupasa uwe unausoma
mchezo mapema kwani si wanawake wote wataweza sema au kujitegesha na
ndio maana tunasisitiza isipite wiki bila kupeana na mwenza wako.
Pia wanawake nawashauri wawe "wachokozi"
kidogo maana kuna wanaume huwa hawaanzi mashambulizi mpaka
washambuliwe, kama hali ipo hivyo basi mwanamke inabidi ndo ume mpangaji
mashambulizi ya awali.
Mwisho niwaambie Mke na Mume, kama inavyowapasa kujua sehemu za
mihemuko baina yenu, inawapasa pia muelewe lugha za miili yenu. Miili
inaongea bwanaa!!!